2 Chronicles 27:1-6

Yothamu Mfalme Wa Yuda

(2 Wafalme 15:32-38)

1 aYothamu alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na sita. Mama yake aliitwa Yerusha binti Sadoki. 2 bAkafanya yaliyo mema machoni pa Bwana kama Uzia baba yake alivyokuwa amefanya, lakini tofauti na yeye, hakuingilia huduma za hekaluni mwa Bwana. Lakini hata hivyo, watu wakaendelea na desturi zao mbaya. 3 cYothamu akajenga upya Lango la Juu la Hekalu la Bwana na kufanya kazi kubwa kwenye ukuta katika kilima cha Ofeli. 4Akajenga miji katika vilima vya Yuda pamoja na ngome na minara mwituni.

5 dYothamu akafanya vita na mfalme wa Waamoni na kumshinda. Mwaka ule Waamoni wakamlipa talanta 100
Talanta 100 za fedha ni sawa na tani 3.75.
za fedha, kori 10,000
Kori 10,000 za ngano ni sawa na tani 2.2.
za ngano na kori 10,000 za shayiri. Waamoni wakamletea kiasi hicho hicho mwaka wa pili na wa tatu.

6 gYothamu akaendelea kuwa na nguvu kwa sababu alienenda kwa ukamilifu mbele za Bwana Mwenyezi Mungu wake.

Copyright information for SwhKC